Mafunzo 7 yaliyomo katika kitabu cha why "A" students work for "C" students and "B"students work for the government
Kila
mmoja kwa nafasi yake angependa kujifunza zaidi kuhusiana na fedha, wapo wengi
ambao hushindwa kutambua ni wapi elimu hii wanaweza kuipata, na wachache
hufanikiwa kuipata katika umri tofauti tofauti wapo wale ambao hufanikiwa
wakiwa na umri mdogo yaani kutokana na mazingira waliyokuzwa nayo na wapo wale
ambao huipata elimu hiii tayari wakisha kuwa wakubwa kiasi cha kujitambua.
Hakika zipo makala mbalimbali ambazo zinazungumzia masuala ya uchumi ama fedha
kwa ujumla, pia vitabu ambavyo huandikwa na watu mashuhuri kama vile Robert
Kiyosaki, Brian Tracy pia Wallace D Wattles na wengineo wengi
Lakini
leo nimekuletea makala ambayo inazungumzia masuala ya upatikanaji wa
fedha kupitia uwezo wetu wa akili na jinsi vile tunaweza kuwaza sisi wenyewe
Makala hii inazungumzia mambo saba ambayo yamekuwa mafunzo yanayotoa elimu ya
fedha na kuwasaidia watu engi mno katika dunia yetu. Kitabu hiki kimeandikwa na
Robert Kiyosaki na kinaitwa "why "A"
students work for "C" students and "B"students work for the
government"
kukipata kitabu hiki kwa mfumo wa pdf bure bofya link hii
hapa chini
Utakapopakua
kitabu hiki utaweza kujifunza mambo mengi sana kuhusu fedha na njia zake za
kuimanage hata isikupotee tena pale uipatapo, na yafuatayo ni mafunzo 7 ambayo
tunayapata ndani ya kitabu hiki
1. kila mtu ni "Genius"
Robert Kiyosaki amekuwa na sababu kubwa sana ya
kusema kwamba katika hii dunia kila mtu ni "Genius" sababu hizi
amezitaja katika sehemu mbalimbali ya kitabu hiki, mwanzo tu alianza kwa kusema
kauli ya Albert Einstein uliosema
"But if
you judge the ability of a fish to climb a tree, it will live its whole
life
believing that it is stupid"
Kwa mantiki hii watu wengi huangahika mfano wa
samaki anyetamani kupanda mti, huku wa wenyewe wakijizani ni wapumbavu kwa
kushindwa kufaulu kwa kila kitu ambacho wanakihitaji, lakini hakika wengi wao
huwa si kosa lao.....
"go to school to get a good job"
muda mwingine huwa wazazi wetu hutuambia maneno
haya ambayo huonesha moja kwa moja kuwa tunaenda kusoma hili tuajiriwe na
kupata pesa tu tofauti na dunia ya leo, Robert asema zaidi kwamba kwanini somo
la pesa halikufundishwa mashuleni endapo kama wote tunaenda shule hili tupate
kazi ambayo itatulipa pesa?
watu wengi huenda shule sehemu ambayo
haifundishi san kuhusiana na kipaji ama "genius" ya mtu mmoja mmoja
na hivyo hupoteza uwezo wao
2. Elimu ni kuhusiana na "content" and "Context"
Elimu
ya kitaaluma ni elimu ambayo imejikita katika content au "maudhui"
tu mfano, ukienda shule unatakiwa ujue kuhusiana na kusoma, kuandika,
mahesabu pasipo na kujali kuwa wewe mwenyewe ni lazima uhusishwe katika
mambo haya hapa mtu ambaye yeye amejaaliwa katika mwili mfano, watu wa riadha
na michezo tofauti hakika hawatoweza kuongoza katika masomo haya ya darasani
"Context"
ni mwanafunzi mwenyewe ambaye shule na elimu inayotoa huwa haimuangalii nini
mwanafunzi huuyu anahitaji
mfano
wapo wanaoenda shule huku wakiamini kuwa watakuja kuwa wafanyabiashara wakubwa
sana duniani lakini mwisho wa siku huangukia na kuwa madaktari sehemu ambayo
hawakuwahi kuwaza kama wangekuwa huko
3. Shule haziwaandai wanafunzi kwa ajili ya kukabiliana na dunia ya halisi
kila
mtoto ni "Genius" lakini kwa bahati mbaya kipaji chake ama
uwezo alionao hauwezi kutambulika kupitia shule zetu ambazo kila siku
hufundisha kitu sawa kwa wanafunzi wote ambao wna ndoto tofauti tofauti na kwa
hali hii hakika huwezi gundua ni nini ama nani utakuwa hapo mbele, niw achache
tu mabao hufanikiwa na wengi wao huishia kuwa tu viongozi wa makampuni fulani
makampuni ambayo wamiliki ni wale mabao hawajamaliza shule au hawakwenda kabisa
shule!!!
Shule
huwafanya wanafunzi wawe washindanaji amabpo hushindania kupata A darasani na
si kuwa wapambanaji au watengenezaji wa ajira katika dunia halisi
4. Elimu ya Uchumi huanza tangu utoto
Jambo
hili ndilo ambalo limemfanya Robert aandike kitabu hiki huku akiwashauri wazazi
kuhusiana na maisha ya kifedha kwa ajili ya watoto wao hapa Robert alimaanisha
kuwa tunatakiwa kuwafundisha watoto wtu tangu wakiwa wadogo kuhusiana na mambo
yote yanayohusiana na pesa, Endapo tutafanya hivi watoto wetu watakuwa ana
uwezo mkubwa wa kukabiliana na dunia iliyo halisi
5. Nini hugharimu mpaka kuwa Tajiri
Watu
wengi huamini kuwa matajiri ni wezi.......japo wapo....
lakini
jambo lililo jema kutambua ni kwamba kila mtu ananweza kuwa Tajiri kulingana na
vile tu mtu atakavyojiweka na kujisumbua kuutafuta huo utajiri watu wengi
hufikia malengo yao ya utajiri kwa kufanya kazi kwa bidii, kutengeneza
biashara, kuweka budget nzuri, kutenegenza ajira zitakazokuletea faida.
Wanafunzi wengi ambao hufanikiwa katika dunia halisi ni wale ambao husoma
mafunzo ambayo hayafundishwi darasani,....
soma maelezo zaidi kutoka kitabu cha
Rich dad Poor dad
6. Nguvu ya lugha
Robert
anaeleza kuwa tangua lipokuwa mdogo kila alipojifunza lugha hakuwahi kufanya
vizuri katika mafunzo hayo ya lugha hila siku moja alipoudhuria katika mkutano
wa baba yake ambaye ni tajiri ndipo aligundua kuwa kwa mtu kuwa tajiri si
lazima ajue lugha nyingi, hila ni uwezo wake wa kutambua tu lugha ya kitaaluma
mfano mtu wa sheria bhasi huwa anaongea kugha ya kisheria, mtu uhasibu huwa
anaongea kugha yake ya kihasibu, hivyo nai vyema sana kujua lugha moja kwa
umakini zaidi ila uijue katika taaaluma tofautitofauti hiyo itasaidia sana
7. Funzo juu ya "mali na madeni"
Robert
anaeleza kuwa katika safari ya kuwa tajiri ni lazima kuweza kutambua juu ya
mali na madeni kwani mali ndiye kitu ama jambo la pekee litakalokufanya uweze
kuingiza pesa kwa wingi, kwa vike unavyomiliki mali nyingi ndvyo hivyo hivyo
utakavyokuwa na uwezo nkubwa wa kupata pesa,,hii ni tofauti sana na mtu mabaye
anakuwa na madeni mengi mno mtu huyu lazima moja kwa moja atakuwa amsikini
akwani kila pesa anayopata bhasi itakuwa inaishia ttu katika kulipa madeni
ambayo anadaiwa.
Shukrani
sana kwa kufatilia makala hii hadi mwisho naamini umejifunza mambo mebgi kutoka
hapa, tuanakuomba uzidi kuwa karibu nasi kwani bado kuna mengi yaliyo mazuri
zaidi ya hili yanakuja
Comments
Post a Comment